Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa s Shirika la Habari la Hawza, Sayyidah Zahra Barqa’i katika kikao kilichofanyika kwa anuani ya “Mwanamke wanafunzi wa dini, ni miongoni mwa mienendo mashuhuri ya Hawza ya Qum” kilichofanyika katika shirika hilo la habari, alisema: Ili kufafanua mafanikio ya Hawza, hususan baada ya Mapinduzi ya Kiislamu, ni muhimu turejee katika historia.
Akaongeza kusema: Katika mwanzo wa Uislamu, mtazamo wa Mtume (s.a.w) kuhusu mwanamke ulikuwa wa kitamaduni wa hali ya juu na wa kimaendeleo. Wakati huo kulikuwepo wanawake wabobezi na wasomi kama vile Bibi Zahra (s.a) na Bibi Khadija (s.a). Bibi Khadija alitambulika kutokana na misaada na huduma alizozitoa kwa ajili ya Uislamu, lakini pia alikuwa na hadhi ya juu katika elimu na itikadi.
Mkurugenzi wa Jami'atu az-Zahra (s) aliendelea kusema: Asmaa, mke wa Ja'far Tayyar, alikuwa miongoni mwa wapokezi wa hadithi. Vilevile Nas'ibah alijulikana kama mwanamke shujaa aliyemtetea Mtume (s.a.w), na pia alikuwa miongoni mwa wapokezi wa hadithi.
Akasema: Baada ya kufariki kwa Mtume (s.a.w), watawala waliokuja madarakani walimweka mwanamke pembeni, jambo ambalo lilisababisha wanawake kutoonekana sana katika masuala ya kielimu. Hata hivyo, kulikuwapo wanawake waliopata maendeleo ya kielimu kutokana na hali zao kibinafsi, za kifamilia na vipaji vyao vya asili, na wakaacha nyuma athari muhimu za kielimu, ingawa idadi yao ilikuwa ndogo sana.
Mkurugenzi wa Jami'atu az-Zahra (s) alisisitiza tena: Moja ya baraka za Hawza ya Qum katika karne hii ya sasa, ni harakati zake pana katika kuanzisha na kuendeleza hawza ya wanawake, jambo ambalo limeleta mafanikio mengi kama vile kulea maelfu ya wanawake waumini, wasomi, wenye kihoro kwa ajili ya dini, wenye haya, wenye maadili mema na waliobobea katika nyanja mbalimbali za tablighi, ufundishaji, utafiti na uongozi, katika kiwango cha kitaifa na hata kimataifa.
Maoni yako